Search
 
 

Display results as :
 


Rechercher Advanced Search

Keywords

Latest topics
» Wema Azua Timbwili Eti Kisa Ally Kiba!
18/3/2015, 8:08 pm by Admin

» Your first subject
18/3/2015, 3:14 am by Admin

January 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar


Wema Azua Timbwili Eti Kisa Ally Kiba!

G6 :: Gossips

Go down

Wema Azua Timbwili Eti Kisa Ally Kiba!

Post by Admin on 18/3/2015, 8:08 pm

Mrembo na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kusababisha timbwili la aina yake hivi karibuni, akidaiwa kuwa kwenye harakati za kutaka kukaa karibu na staa wa Bongo Fleva , Ally Kiba.

Kwa mujibu wa gazeti la Risasi Mchanganyiko, tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Triple A, jijini Arusha ambapo Wema alienda kwenye sherehe ya mmoja wa rafiki zake huku yeye akipewa ‘taito’ ya mgeni rasmi.

Chanzo cha gazeti hilo kilidokeza kuwa hivi karibuni, Kiba alikuwa na shoo maalum mjini Arusha ambayo ilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo ambapo siku hiyohiyo, Wema naye alikuwa na marafiki zake wakisherehekea na wenyeji wake, hivyo baada ya kuisha na kusikia Kiba yupo mjini hapo, akaona ni fursa nzuri ya kwenda kumuona.

“Wema alialikwa na rafiki yake mmoja hivi huku Arusha sasa baada ya sherehe yao kuisha na kuambiwa Kiba anaangusha shoo, akaona bora aibuke Triple A akamuone,” kilisema chanzo hicho.

Katika aya nyingine, chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, Wema aliamua kwenda kwenye shoo hiyo ya Kiba akiamini atamrusha roho zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye anadaiwa kuwa haziivi na Kiba.
“Nasikia Wema alitaka kwenda ukumbini ili ikiwezekana apige mapicha ya kumwaga na Ali Kiba ili yakivuja yamuumize Diamond,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baadhi ya wapambe wa Kiba (Team Kiba) waliposhtukia mchezo huo, walimzuia Wema getini ili asiweze kuonana naye.

“Wema alikuja majira ya saa 7:45 usiku akiwa na timu yake, kufika pale walitaka kuingia, lakini kwa hali aliyokuwa nayo wakakataa kumruhusu. “Walijua lazima angefanya kitu kwa Kiba, kitendo ambacho wao hawakupenda, hivyo mabaunsa wakafanya kazi yao vizuri.

“Kitendo cha kumkatalia kuingia kilisababisha kizaazaa hasa kutoka kwa wapambe wake. Ilitokea patashika nguo kuchanika kabla ya kukubali yaishe na kuondoka zao,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuvutiwa waya na kusomewa mashtaka, Wema alitiririka; “Ni kweli nilikuwa Arusha kwa shughuli zangu, nilifikia Mount Meru ambayo pia baadaye Kiba naye alifikia na tulionana, usiku kulikuwa na pati ya marafiki zangu, tukawa huko tulipomaliza tukaenda kwenye shoo ya Kiba.

“Kwa kweli sikumbuki chochote maana siku hiyo nilikuwa nimelewa sana, kwa hiyo nashindwa kusema kama unachosema nilikifanya au la, ila kesho yake niliambiwa kuwa tulikwenda kwenye shoo ya Kiba na hatukuingia.
“Hata wakati wa kurudi hotelini kwetu sikujua nilifikaje, zaidi ya kesho yake asubuhi niliwasikia kina Martin wakisema kwamba tulienda Triple A lakini kweli hatukuingia kutokana na fujo zilizokuwa zimejitokeza pale hivyo tukaamua kurudi kulala.”
avatar
Admin
Admin

Posts : 2
Join date : 2015-03-18

View user profile http://feisal.board-directory.net

Back to top Go down

Back to top

- Similar topics

G6 :: Gossips

 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum